Matangazo

Imewekwa: Nov 03, 2020

KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA TAREHE 25 NOVEMBA - 10 DESEMBA

KAULIMBIU YA MWAKA 2021

EWE MWANANCHI: KOMESHA UKATILI WA KIJINSIA SASA

Chimbuko la maadhimisho haya limetokana Tamko la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa awamu ya saba, Kofi Annan la mwaka 2006 la kutaka Dunia itambue kuwa lipo tatizo kubwa la ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na watoto wa kike, hivyo kuna umuhimu wa kuwa na kipindi maalum cha Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia ambayo ilikubaliwa ifanyike kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Desemba kila mwaka. Lengo la kampeni hii ni kuongeza ushawishi, kubadilishana taarifa na uzoefu, kujenga uwezo wa pamoja, matumizi mazuri ya rasrimali zinazopatikana na kuunganisha nguvu za asasi za kijamii katika kuhamasisha, kuelimisha, kukemea na kuchukua hatua kwa pamoja ili kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii