Matangazo

Imewekwa: Jun 03, 2020

Taarifa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali

TAARIFA KWA UMMA

Tunayajulisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyoorodheshwa hapa chini kuwa yamekiuka vigezo na masharti ya usajili kama ifuatavyo:-

  • (i)Kushindwa kuwasilisha taarifa za mwaka kinyume na kifungu cha 29(1) (a) na (b) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002;
  • (ii)Kushindwa kulipa malipo ya ada elekezi kinyume na kifungu cha 38(2)(b) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na 24 ya mwaka 2002, ikisomwa pamoja na Kanuni ya 10 ya Kanuni ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2004 na jedwali la pili la Kanuni ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2014.

HIVYO ZINGATIA kwamba, Mashirika hayo yanapaswa kuwasilisha utetezi wake ndani ya siku 14 juu ya kwanini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yake.

Orodha ya Mashirika hayo pia inapatikana katika tovuti ya Wizara www.jamii.go.tz na tovuti ya Idara www.tnnc.go.tz

Vickness G. Mayao

MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

02.06.2020

Tanzania Census 2022