Matangazo

 • ​TARATIBU ZA KUSAJILI MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs) TANZANIA BARA

  TARATIBU ZA KUSAJILI MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs) TANZANIA BARA

  A. MASHIRIKA YA NDANI YA NCHI (LOCAL NGO):-

  (i) Lazima kuwe na watu wasiopungua watano (5) wote watanzania;

  (ii) Kuwasilisha Katiba itakayosajiliwa;

  (iii) Kuwasilisha Muhtasari wa kikao uliosainiwa na wanachama waanzislishi;

  (iv) Kuwasilisha barua ya utambulisho (Recommendation Letter) kutoka kwa Msajili Msaidizi wa Halmashauri au Mkoa Ofisi ilipo.

  B. MASHIRIKA YA KIMATAIFA (INTERNATIONAL NGO)

  (i) Kuwa na watu wasiopungua watano (5) ambapo kati yao angalau wawili lazima wawe Watanzania;

  (iii) Kuwasilisha nakala ya katiba ya usajili kutoka nchi iliposajiliwa;

  (iv) Kuwasilisha nakala ya cheti cha usajili kutoka nchi ilikosajiliwa;

  (v) Kuwasilisha Muhtasari wa kikao cha wanachama waanzilishi;

  (vi) Kuwasilisha barua ya utambulisho (Recomendation Letter) kutoka kwa Msajili Msaidizi wa Halmashauri au Mkoa Ofisi ilipo.

  NB: Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (Local & International - NGOs), hufanyika kwa njia ya mfumo wa kielekroniki kupitia tovuti: nis.jamii.go.tz

  C. ADA ZA USAJILI

  Mashirika ya Kimataifa - USD 350

  Mashirika ya Ndani :-

  • Ngazi ya Kitaifa - Tsh. 115,000/=
  • Ngazi ya Mkoa - Tsh. 100,000/=
  • Ngazi ya Wilaya - Tsh. 80,000/=
  • Ushuru wa Stempu za TRA; Shirika la ndani (Stamp Duty) - Tsh. 1,500/=
  • Ushuru wa Stempu za TRA; Shirika la Kimataifa (Stamp Duty) - Tsh. 4,500/=

  D. MAHITAJI BAADA YA USAJILI

  (i) Kulipa Ada ya mwaka 50,000/= kwa Mashirika ya ndani na $100 kwa Mashirika ya Kimataifa. Malipo ni sambamba na uwasilishaji wa Ripoti za Mwaka za Utendaji kazi pamoja naTaarifa ya Fedha iliyokaguliwa. Malipo hufanyika kati ya Tarehe 01 Januari hadi 15 Aprili. Kushindwa kutimiza takwa hili la kisheria hupelekea kulipa faini ya Tsh. 100,000/= kwa Mashirika ya Ndani na $300 kwa Mashirika ya Kimataifa.

  (ii) Shirika ambalo litashindwa kulipa ada na kushindwa kuwasilisha taarifa za mwaka za utendaji kazi kwa miaka miwili mfululizo litakuwa limepoteza sifa za usajili na litatakiwa kufutwa kwa mujibu wa sheria.

  ... Soma zaidi

  Imewekwa: Jan 10, 2024

 • KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2023/2024 KWA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII NA MAENDELEO YA JA

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM


  S.L.P 573 DODOMA Tovuti: www.jamii.go.tz

  …………………………………………………………………………………………………….

  TAARIFA KWA UMMA

  KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2023/2024 KWA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII NA MAENDELEO YA JAMII UFUNDI

  Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum inapenda kuwatangazia Watanzania kuwa udahili kwa mwaka wa masomo 2023/2024 kwa mujibu wa tangazo la Baraza la taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) udahili utaanza tarehe 15 MEI 2023 kwa waombaji ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa wenye kukidhi vigezo na sifa kwa kozi mbalimbali nchini zitolewazo na Vyuo.

  Wizara kupitia Vyuo vyake vya Maendeleo ya Jamii (Buhare,Monduli,Ruaha, Mlale, Uyole na Rungemba) na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ufundi (Misungwi na Mabughai) wanapokea maombi kuanzia tarehe21 MEI, 2023 hadi 30 JUNI 2023 awamu ya kwanza kwa programu za Maendeleo ya Jamii (Community Development) na Uhandisi Ujenzi na Maendeleo ya Jamii (Civil Engineering with Community Development) kwa ngazi ya Cheti cha Awali, Astashahada na Stashahada (Basic Technician Certificate(NTA Level 4),Technician Certificate(NTA Level 5) and Ordinary Diploma(NTA Level 6)

  Maombi yote yatafanyika kwa namna tofauti kama ifuatavyo

  • 1.Kupakua fomu za Maombi kupitia tovuti ya Wizarawww.jamii.go.tz au tovuti za chuo husika kama zinavyoonekana hapo chini na kisha kuzituma kwa sanduku la posta au baruapepe ya chuo husika
  • 2.Kufika chuoni moja kwa moja na sifa za mwombaji kwa ajili ya kujaza fomu kwa waombaji waliokaribu na chuo husika
  • 3.Kujaza fomu za maombi kwa njia ya mtandao- online application kupitia tovuti ya chuo husika

  Wizara inatoa wito kwa wahitimu wa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita na waliomaliza VETA NVA Level III kujiunga na programu zetu kwa kuwa ni programu zenye tija kwa muombaji na Taifa kwa ujumla kwani Taifa lolote linaloendelea lazima liwe na wataalam wenye ujuzi na maarifa unaolingana na mahitaji ya soko kwa sasa na wenye ari na morali ya kulijenga Taifa.


  Kwa maelezo zaidi wasiliana

  A. VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII (COMMUNITY DEVELOPMENT TRAINING INSTITUTEs)

  BUHARE CDTI

  Postal Address: P.O.Box 190 Musoma Mara

  Email Address: pbuhare@jamii.go.tz

  Website: www.buharecdti.ac.tz

  Principal Phone Number :0752760981

  Vice principal Academic : 0753783945

  Admission Officer0625908044

  Account Number & name: 30301100002 Economic Account Community Development Training Institute NMB

  MONDULI CDTI

  Postal Address: P.O.Box 45 monduli Arusha

  EmailAddress:pmonduli@jamii.go.tz

  Website: www.cdtimonduli.ac.tz

  Principal Phone Number :0762740341

  Vice principal Academic : 0759228112

  Admission Officer0757156866

  Account Number & name: 41301100018 Principal CDTI MonduliNMB

  RUAHA CDTI

  Postal Address: P.O.Box 254 Iringa

  EmailAddress:pruaha@jamii.go.tz

  Website: www.ruahacdti.ac.tz

  Principal Phone Number :0787080646

  Vice principal Academic : 0752568016

  Admission Officer0717767549

  Account Number & name: 60510000812 Ruaha CDTI NMB

  MLALE CDTI

  Postal Address: P.O.Box 86 Songea

  EmailAddress:pmlale@jamii.go.tz

  Website: www.mlalecdti.ac.tz

  Principal Phone Number :0712719534

  Vice principal Academic : 0713457522

  Admission Officer0658882009

  Account Number & name: 61802300241 Mlale CDTI Selfreliance project fundNMB

  UYOLE CDTI

  Postal Address: P.O.Box 1343 MBEYA

  EmailAddress:puyole@jamii.go.tz

  Website: www.cdtiuyole.ac.tz

  Principal Phone Number :0754576455

  Vice principal Academic : 0755047572

  Admission Officer0685047572

  Account Number & name: 61010022274 CDTI Uyole –Other CollectionNMB

  RUNGEMBA CDTI(For female applicants only)

  Postal Address: P.O.Box 6 Mafinga Iringa

  EmailAddress:prungemba@jamii.go.tz

  Website: www.rungembacdti.ac.tz

  Principal Phone Number :0783334545

  Vice principal Academic : 0783955256

  Admission Officer0769493600

  Account Number & name: 60202300255 Rungemba Economic Activities NMB

  B: VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII UFUNDI (COMMUNITY DEVELOPMENT TECHNICAL TRAINING INSTITUTEs)

  Misungwi Community Development Technical Training Institute –Mwanza

  Mabughai Community Development Technical Training Institute –Tanga

  Postal Address: P.O.Box 2799 Mwanza

  Email Address: pmissungwi@jamii.go.tz

  Website : www.misungwicdtti.ac.tz

  Principal Phone Number :0767040803

  Vice principal Academic : 0713197574/0743520523

  Admission Officer: 0653118018/0744586637

  Admission officer email address: misungwicdtti@gmail.com

  Account Number& Name: 31301100002CDTTI Mafunzo NMB

  Postal Address: P.O.Box 111 Lushoto Tanga

  Email Address: pmabughai@jamii.go.tz

  Website : www.jamii.go.tz

  Principal Phone Number :0753606644

  Vice principal Academic : 0759509439/0654551341

  Admission Officer: 0767913070/0653619495

  Admission officer email address: pmabughai@jamii.go.tz

  Account Number& Name: 41602301399UzalishajiMabughai CDTTINMB

  IMETOLEWA NA:

  WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM

  TAREHE: 25/05/2023

  ... Soma zaidi

  Imewekwa: May 26, 2023

 • TAARIFA MUHIMU

  Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anayatangazia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kuwasilisha taarifa zao za mwaka 2022 na kulipa ada kuanzia tarehe 01 Januari, 2022. Ada ya mwaka ni Shilingi 50,000/= kwa Mashirika ya Ndani (Local NGOs) na USD 100 kwa Mashirika ya Kimataifa (International NGOs). Mwisho wa kuwasilisha taarifa na kulipa ada ya mwaka 2022 ni tarehe 15.4.2022 saa 6: 00 Usiku. Baada ya tarehe hiyo malipo yote ya ada yatalipwa na faini ya TShs.100,000/= kwa Mashirika ya Ndani (Local NGOs) na USD 300 kwa Mashirika ya Kimataifa (International NGOs).

  Taarifa hizo ziwasilishwe kupitia mfumo wa usajili wa NGOs (nis.jamii.go.tz) kwa kutumia akaunti za Mashirika. Aidha, kwa wale wasio na Akaunti kwenye mfumo waombe kupitia jamii.go.tz katika kipengele cha NGOs MIS na kisha kujaza fomu kiufasaha na kuiwasilisha kwenye mfumo. Hautatolewa muda wa ziada wa kuwasilisha taarifa, na kutowasilisha taarifa ni kinyume na kifungu cha 29(1) (a) na (b) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na.24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005 na 2019.

  MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI Tel: 0737 569 583/ 0737 569 584/0762 361 646 12 Disemba, 2022 _____________

  ... Soma zaidi

  Imewekwa: Dec 21, 2022

 • TAARIFA MUHIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII

  TAARIFA MUHIMU

  Wizara inawatangazia wanafunzi wote wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vya Uyole, Rungemba, Ruaha, Buhare, Mlale na Monduli na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ufundi vya Misungwi na Mabughai kuwa matokeo ya Muhula wa pili kwa mwaka wa masomo 2021/2022 yametoka na yanapatikana katika tovuti www. jamii.go.tz na tovuti za Vyuo husika. Wanafunzi ambao hawajafanya mitihani ya muhula wa kwanza watafanya mitihani maalum (special examination) baada ya muhula wa pili kukamilika.

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

  ... Soma zaidi

  Imewekwa: Aug 19, 2022

 • TAARIFA MUHIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII

  TAARIFA MUHIMU

  Wizara inawatangazia wanafunzi wote wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vya Uyole, Rungemba, Ruaha, Buhare, Mlale na Monduli na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ufundi vya Misungwi na Mabughai kuwa matokeo ya Muhula wa pili kwa mwaka wa masomo 2021/2022 yametoka na yanapatikana katika tovuti www. jamii.go.tz na tovuti za Vyuo husika.Wanafunzi ambao hawajafanya mitihani ya muhula wa kwanza watafanya mitihani maalum (special examination) baada ya muhula wa pili kukamilika.

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

  ... Soma zaidi

  Imewekwa: Aug 19, 2022

 • KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023 KWA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII NA VYUO VYA MAENDE

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM


  S.L.P 573 DODOMA Tovuti: www.jamii.go.tz

  …………………………………………………………………………………………………….

  TAARIFA KWA UMMA

  KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023 KWA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII NA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII UFUNDI

  Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum inapenda kuwatangazia Watanzania kuwa udahili kwa mwaka wa masomo 2022/2023 kwa mujibu wa tangazo la Baraza la taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) udahili utaanza tarehe 24 MEI 2022 kwa waombaji ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa wenye kukidhi vigezo na sifa kwa kozi mbalimbali nchini zitolewazo na Vyuo.

  Wizara kupitia Vyuo vyake vya Maendeleo ya Jamii (Buhare,Monduli,Ruaha, Mlale, Uyole na Rungemba) na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ufundi (Misungwi na Mabughai) wanapokea maombi kuanzia tarehe24 MEI, 2022 hadi tarehe 30 JULAI 2022 kwa programu za Maendeleo ya Jamii (Community Development) na Uhandisi Ujenzi na Maendeleo ya Jamii (Civil Engineering with Community Development) kwa ngazi ya Cheti cha Awali, Astashahada na Stashahada (Basic Technician Certificate(NTA Level 4),Technician Certificate(NTA Level 5) and Ordinary Diploma(NTA Level 6)

  Maombi yote yatafanyika kwa namna tofauti kama ifuatavyo

  • 1.Kupakua fomu za Maombi kupitia tovuti ya Wizarawww.jamii.go.tz au tovuti za chuo husika kama zinavyoonekana hapo chini na kasha kuzituma kwa sanduku la posta au baruapepe ya chuo husika
  • 2.Kufika chuoni moja kwa moja na sifa za mwombaji kwa ajili ya kujaza fomu kwa waombaji waliokaribu na chuo husika
  • 3.Kujaza fomu za maombi kwa njia ya mtandao- online application kupitia tovuti ya Chuo husika

  Wizara inatoa wito kwa wahitimu wa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita na waliomaliza VETA NVA Level III kujiunga na programu zetu kwa kuwa ni programu zenye tija kwa muombaji na Taifa kwa ujumla kwani Taifa lolote linaloendelea lazima liwe na wataalamu wenye ujuzi na maarifa unaolingana na mahitaji ya soko kwa sasa na wenye hari na morali ya kulijenga Taifa.


  Kwa maelezo zaidi wasiliana

  A. VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII (COMMUNITY DEVELOPMENT TRAINING INSTITUTEs)

  BUHARE CDTI

  Postal Address: P.O.Box 190 Musoma Mara

  Email Address: pbuhare@jamii.go.tz

  Website: www.buharecdti.ac.tz

  Principal Phone Number :0752760981

  Vice principal Academic : 0753783945

  Admission Officer0625908044

  Account Number & name: 30301100002 Economic Account Community Development Training Institute NMB

  MONDULI CDTI

  Postal Address: P.O.Box 45 monduli Arusha

  EmailAddress:pmonduli@jamii.go.tz

  Website: www.cdtimonduli.ac.tz

  Principal Phone Number :0762740341

  Vice principal Academic : 0759228112

  Admission Officer0757156866

  Account Number & name: 41301100018 Principal CDTI MonduliNMB

  RUAHA CDTI

  Postal Address: P.O.Box 254 Iringa

  EmailAddress:pruaha@jamii.go.tz

  Website: www.ruahacdti.ac.tz

  Principal Phone Number :0787080646

  Vice principal Academic : 0752568016

  Admission Officer0717767549

  Account Number & name: 60510000812 Ruaha CDTI NMB

  MLALE CDTI

  Postal Address: P.O.Box 86 Songea

  EmailAddress:pmlale@jamii.go.tz

  Website: www.mlalecdti.ac.tz

  Principal Phone Number :0712719534

  Vice principal Academic : 0713457522

  Admission Officer0658882009

  Account Number & name: 61802300241 Mlale CDTI Selfreliance project fundNMB

  UYOLE CDTI

  Postal Address: P.O.Box 1343 MBEYA

  EmailAddress:puyole@jamii.go.tz

  Website: www.cdtiuyole.ac.tz

  Principal Phone Number :0754576455

  Vice principal Academic : 0755047572

  Admission Officer0685047572

  Account Number & name: 61010022274 CDTI Uyole –Other CollectionNMB

  RUNGEMBA CDTI(For female applicants only)

  Postal Address: P.O.Box 6 Mafinga Iringa

  EmailAddress:prungemba@jamii.go.tz

  Website: www.rungembacdti.ac.tz

  Principal Phone Number :0783334545

  Vice principal Academic : 0783955256

  Admission Officer0769493600

  Account Number & name: 60202300255 Rungemba Economic Activities NMB

  B: VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII UFUNDI (COMMUNITY DEVELOPMENT TECHNICAL TRAINING INSTITUTEs)

  Misungwi Community Development Technical Training Institute –Mwanza

  Mabughai Community Development Technical Training Institute –Tanga

  Postal Address: P.O.Box 2799 Mwanza

  Email Address: pmissungwi@jamii.go.tz

  Website : www.misungwicdtti.ac.tz

  Principal Phone Number :0767040803

  Vice principal Academic : 0713197574/0743520523

  Admission Officer: 0653118018/0744586637

  Admission officer email address: misungwicdtti@gmail.com

  Account Number& Name: 31301100002CDTTI Mafunzo NMB

  Postal Address: P.O.Box 111 Lushoto Tanga

  Email Address: pmabughai@jamii.go.tz

  Website : www.jamii.go.tz

  Principal Phone Number :0753606644

  Vice principal Academic : 0759509439/0654551341

  Admission Officer: 0767913070/0653619495

  Admission officer email address: pmabughai@jamii.go.tz

  Account Number& Name: 41602301399UzalishajiMabughai CDTTINMB

  IMETOLEWA NA:

  IDARA YA TEHAMA

  ... Soma zaidi

  Imewekwa: Jun 03, 2022

 • HATI YA KUKUSUDIA KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

  Hii ni kujulisha kuwa umekiuka sheria na masharti ya usajili kama hapa chini:-

  (I) Kushindwa kuwasilisha ripoti ya mwaka kwa miaka miwili mfululizo kinyume na kifungu cha 29 (1) (a) na (b) cha sheria ya Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali Na. 24 ya 2002;

  (II) Kushindwa kulipa ada za mwaka za Shirika Kinyume na kifungu cha 38(2) (b) cha sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na. 24 of 2002 kinachosomwa pamoja na Kanuni ya 10 ya Kanuni ya Kanuni za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2004 na Jedwali la Pili la Kanuni Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (Marekebisho) ya 2014.

  UNAARIFIWA kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 24 9(1) na (2) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya 2002, unatakiwa kutoa sababu zinazojitosheleza kwa maandishi kwa ofisi ya Msajili kabla ya tarehe 30 Juni, 2022.

  Orodha ya Masharika yanayokusudiwa kufutwa yanapatikana kwenye tovuti www.jamii.go.tz

  Vickness G.Mayao

  MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

  ... Soma zaidi

  Imewekwa: May 09, 2022

 • ​TAARIFA MUHIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII

  TAARIFA MUHIMU

  Wizara inawatangazia wanafunzi wote wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vya Uyole, Rungemba, Ruaha, Buhare, Mlale na Monduli na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ufundi vya Misungwi na Mabughai kuwa matokeo ya Muhula wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2021/2022 yametoka na yanapatikana katika tovuti www. jamii.go.tz na tovuti za Vyuo husika.

  Wanafunzi ambao hawajafanya mitihani ya muhula wa kwanza watafanya mitihani maalum (special examination) baada ya muhula wa pili kukamilika.

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

  ... Soma zaidi

  Imewekwa: Apr 01, 2022

 • INVITATION TO PARTICIPATE IN THE STAKEHOLDERS MEETING

  The Ministry of Community Development, Gender, women and Special Groups would like to appreciate for your continued support in various interventions and initiatives organized by the Ministry.

  The Ministry is organizing a one – day stakeholders meeting to be held on 26th February, 2022 at Morena Hotel Dodoma. The objective of this meeting is to discuss on the National Plan of Action to end Violence against Women and Children (NPA – VAWC) and its Coordination Guideline for the purpose of accelerating implementation of intervention to end violence against women and children.

  In this regard, The ministry would like to invite your good office to participate in the said meeting. The registration link (form) is available at www.jamii.go.tz

  ... Soma zaidi

  Imewekwa: Feb 18, 2022

 • TANGAZO KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs)

  TANGAZO KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs)

  Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) anayatangazia Mashirika yaliyosajiliwa na yanayofanya shughuli zao katika Mikoa ya Dodoma, Singida na Iringa kwamba, Wizara itafanya kikao na viongozi wa Mashirika hayo Mkoani Dodoma. Kikao hicho kitafanyika tarehe 05 Februari, 2022 kuanzia 2.30 asubuhi kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

  Lengo la kikao hicho ni kuzungumzia masuala ya utendaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na nafasi yao katika kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali katika Jamii.

  Aidha, Ofisi ya Msajili itaendesha zoezi la uhakiki na kubadili vyeti vya zamani vya NGOs na kutoa vyeti vipya vyenye ukomo wa miaka kumi (10) kwa NGOs zilizosajiliwa katika Mkoa wa Dodoma, Singida na Iringa kulingana na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 (Sura 56) kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 3 ya mwaka 2019. Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Dodoma kuanzia tarehe 05 hadi 11 Februari, 2022 (saa 2.30 asubuhi hadi saa 11.00 jioni).

  Ili kufanikisha zoezi hilo, Kiongozi au Mwanachama wa NGO anapaswa kufika na nyaraka zifuatazo:

  (i)Cheti halisi (Original) na nakala ya cheti hicho.

  (ii)Orodha ya Wanachama na saini zao;

  (iii)Wasifu (Curriculam Vitae) wa viongozi watatu wa Shirika pamoja na Namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA)-kwa Wanzania na nakala ya pasi ya kusafiria (Passport) kwa raia wa kigeni;

  (iv)Katiba iliyogongwa mhuri wa Ofisi ya Msajili;

  (v)Nakala ya risiti ya malipo ya ada ya mwaka (annual subscription fees) kwa mwaka 2018, 2019, 2020 na 2021.

  (vi)Muhtasari wa wanachama uliopitishwa kama/endapo kuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika hivi karibuni.

  Vickness G. Mayao

  MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

  Simu: 0737 569 583/ 0737 569 584

  ... Soma zaidi

  Imewekwa: Feb 01, 2022