Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

WAZIRI GWAJIMA ASISITIZA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA SIASA

Imewekwa: 31 Jan, 2025
WAZIRI GWAJIMA ASISITIZA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA SIASA


Na WMJJWM – Dar Es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amehimiza Jamii kuimarisha ushiriki wa Wanawake katika Siasa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake (2023), ambayo inaelekeza kuwa na fursa sawa kisiasa na kiuchumi.

Dkt. Gwajima amesema hayo Leo Januari 30, 2025, baada ya kushiriki maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Brigid yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.

Amepongeza uhusiano wa Tanzania na Ireland uliodumu kwa muda mrefu ambao pamoja na mambo mengine umeimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.

"Ni muhimu kuendelea kuondoa vikwazo vinavyowazuia wanawake kushiriki kikamilifu katika uongozi na maamuzi," amesema Waziri Gwajima.

Kwa upande wake, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Nicola Brennan, amesema: "Ireland inaendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha wanawake wanapata fursa sawa katika jamii na siasa na kuleta matokeo chanya katika kwa wanawake nchini Tanzania.

Maadhimisho hayo hufanyika kwa heshima ya Mtakatifu Brigid, ambaye ni mmoja wa watakatifu wakuu wa Ireland, anayejulikana kwa mchango wake katika elimu, haki za wanawake, na uongozi wa kiroho.

Maadhimisho ya Mtakatifu Brigid nchini Tanzania yameadhimishwa kwa mara ya tatu yakitanguliwa na yale yaliyofanyika mwaka 2023 na 2024 na mwaka huu yanangazia kutatua changamoto zinazowakabili Wanawake katika ushiriki wa firasa za kiuchumi na Siasa na namna ya kuzitatua.