Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

WAZIRI DKT. GWAJIMA APONGEZA WIZARA YA MAMBO YA NDANI, JESHI LA POLISI KWA KUWAOKOA WATOTO WALIOTUMIKISHWA KINGONO

Imewekwa: 19 Feb, 2025
WAZIRI DKT. GWAJIMA APONGEZA WIZARA YA MAMBO YA NDANI, JESHI LA POLISI KWA KUWAOKOA WATOTO WALIOTUMIKISHWA KINGONO

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amepongeza Jeshi la Polisi na uongozi wa mkoa wa Ruvuma kwa kuwaokoa watoto wawili wa kike (majina yamehifadhiwa) wenye umri wa miaka 16, waliokuwa wamesafirishwa kutoka kijiji cha Mkowela, Tunduru, hadi machimbo ya Mbinga kwa ahadi ya kupewa kazi za ndani (house girl).

Baada ya kufikishwa Mbinga bosi wao aliwapa kazi ya kuuza baa kisha akiwatumikisha kingono. Baada ya watoto hao kufanyiwa vitendo hivyo wakatoa taarifa kwa wazazi wao kuomba msaada, na taarifa hizo zilimfikia Waziri Gwajima ndipo akawasiliana na Uongozi wa Jeshi la Polisi Mbinga na kufanikiwa kuokolewa kwa watoto hao. 

Waziri Gwajima pia amepongeza mtu aliyetoa taarifa hiyo kupitia mtandao wa X (zamani Twita) anayefahamika kwa jila la Hofa_Remmy16.

Aidha amewahimiza wazazi kuwa makini na watu wanaochukua watoto wao kwa ahadi za ajira, pamoja na kushirikiana na serikali za mitaa kufichua matukio ya ukatili dhidi ya watoto.