WAKILI MPANJU AHITIMISHA KIKAO KAZI CHA WAKUU WA VITENGO VYA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
Na Evelina Odemba WMJJWMM, Morogoro
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju, amehitimisha kikao kazi cha wakuu vitengo vya maendeleo ya Jamii ngazi ya Mkoa.
Wakili Mpanju amefunga kikao kazi hicho tarehe 3 Julai, 2026 Mkoani Morogoro kwa kuwasisitiza washiriki wote kwenda kutekeleza yote ambayo yameazimiwa ndani ya kikao hiko.
"Kupitia kikao hiki wote tumejitathimini na kuona namna gani tunaingia kwenye utekelezaji wa DIRA2050, tukalete matokeo ya maelekezo 10 ya Mhe. Waziri Dkt Gwajima, maeneo ya kimkakati aliyoyaeleza Katibu Mkuu Eliakim Maswi na maazimio 14 ambayo mmeyaazimia ndani ya kikao hiki" amesema Wakili Mpanju.
Aidha naye Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Bora na Maendeleo ya Jamii kutoka OWM - TAMISEMI Stephen Motambi amesisitiza wataalamu hao kufanya kazi hiyo kwa moyo wa kujituma ili kufanikisha maazimio yote yaliyowekwa kwenye kikao.
Awali wakati akitoa salam za utangulizi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Grace Mbwilo amewapongeza washiriki wote kwa kuazimia kuwa na makakati wa pamoja ili kuifikia DIRA ya Maendeleo ya Taifa 2050.