TANZANIA NA NORWAY KUKUZA USAWA WA KIJINSIA.

Na WMJJWM – Dar Es Salaam
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi na Ubalozi wa Norway nchini imekubaliana kushirikiana na kukuza usawa wa kijisnia nchini kupitia Programu ya Gender Equality for Development inayoratibu masula ya usawa wa kijinsia.
Hayo yamebainika Januari 21, 2025 katka kikao kilichowakutanisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Amon Mpanju na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tine Tonnes, katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, kujadili maeneo ambayo Tanzania na nchi ya Norway zinaweza kushirikiana kukuza usawa wa kijinsia.
Mpanju ameishukuru Serikali ya Norway na kuahidi Wizara itaendelea kushirikiana na Ublaozi wao ncini ili kuhakikisha Programu hiyo inaleta ustawi na maendeleo ya watanzania.
Naye Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe, Tine Tonnes amesema Kurugenzi ya masuala ya Watoto, Vijana na Familia nchini Norway (Norwegian Directorate for Children, Youth and Family Affairs) kutoka Norway inayoratibu masula ya usawa wa kijinsia ikiwemo Programu ya Gender Equality for Development, itafanya ziara nchini tarehe 10 na 11 Februari, 2025, ambapo watakutana na wataalam wa Wizara kujadili maeneo ya ushirikiano kulingana na mahitaji yaliyoanishwa.