Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MPANJU AWATAKA WAKAZI WA KIGOMA KUJITOKEZA KATIKA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA.

Imewekwa: 27 Jan, 2025
MPANJU AWATAKA WAKAZI WA KIGOMA KUJITOKEZA KATIKA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amesema Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ni moja ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kupambana na Ukatilia Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA- 2023/24-2028/29) unaohimiza kupambana na mila na desturi zenye madhara ambazo zikiendekezwa zinasababisha kukiukwa kwa haki za wanawake, watoto na makundi maalum.

Mpanju amesema hayo Januari 24, 2025 mkoani Kigoma wakati akitoa salamu katika uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Suluhu Hassan ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.

Akizindua Kampeni hiyo Dkt. Ndumbaro amesema Kampeni ya Msaada wa Kisheria itatekelezwa kwa muda wa siku tisa katika Halmashauri tisa za Mkoa wa Kigoma na kuwafikia Wananchi katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha matatizo yote ya Kisheria yanapatiwa suluhu.