Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

KAMISHANA WA USTAWI WA JAMII ATAKA KUONGEZWA NGUVU AFUA ZA WATOTO

Imewekwa: 28 Jul, 2025
KAMISHANA WA USTAWI WA JAMII ATAKA KUONGEZWA NGUVU AFUA ZA WATOTO

Na WMJJWM- Dar Es Salaam.

Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Nandera Mhando amewataka wadau wanaotekeleza afua za Watoto kuongeza nguvu na kudhibiti Watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani.

Dkt. Nandera ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kuratibu Afua za Watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani
amesema hayo Julai 25, 2025, katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya kamati hiyo.

Kabla ya kikao hicho, kamati imetembelea dawati la huduma za Ustawi wa Jamii katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam kwa lengo
na kutathimini utoaji wa huduma za ustawi kwa watoto.

Dkt. Nandera amesema ni muhimu kwa wadau wote wanaotekeleza Afua za Watoto kuhakikisha wanatoa huduma stahiki kwa mujibu wa sheria na miongozo iliyopo ili tuweze kubailiana na changamoto ya Watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaan.

Dkt. Nandera amesema miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati hiyo na wadau ambao wanahusika katika kuzuia na kuokoa watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani.

"Kamati imejadili njia za ugemaji fedha kutoka kwa wadau ili kusaidia kuboresha utoaji wa huduma za ustawi kwa Watoto ikiwemo makao ya Watoto katika maeneno mbalimbali nchini." amesema Dkt. Nandera

Naye Mjumbe wa Kamati hiyo Mkaguzi wa Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam Mdathiru Kato Makori amesema Jeshi la Polisi linaendelea na operesheni mbalimbali katika vituo vya mabasi ili kuwabaini watoto wanaoishi na kufanya kazi katika maeneo hayo na kuwaokoa kwa kushirikiana na Maafisa Ustawi wa Jamii.

Aidha Mkaguzi wa Polisi Kato ametoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano pamoja na wazazi kutimiza wajibu wa malezi kwa Watoto ili kuzuia wimbo la watoto kuishi na kufanya kazi mtaani.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii Mkoa wa Dar Es Salaam Nyamara Elisha amesizitiza wananchi kuripoti matukio yote ya unyanyasaji na utesaji unaofanywa kwa watoto katika mitaa ili kusaidia vyombo vya sheria kuchukua hatua kwa wote wanaobainika kufanya vitendo hivyo.