Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

KAMATI YAPONGEZA UJENZI WA UKUMBI WA MIKUTANO CHUO CHA USTAWI WA JAMII KIJITONYAMA

Imewekwa: 20 Mar, 2025
KAMATI YAPONGEZA UJENZI WA UKUMBI WA MIKUTANO CHUO CHA USTAWI WA JAMII KIJITONYAMA

NA WMJJWM - Dar Es Salaam

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeridhishwa na kupongeza mradi wa ujenzi wa jengo la ukumbi wa mihadhara lenye uwezo wa kuchukua watu 400 katika Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kampasi ya Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa katika kikao cha majumuisho kilichofanyika Machi 17, 2025, baada ya Kamati hiyo kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, ikihitimisha ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatma Toufiq, ameipongeza Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kusimamia kwa ufanisi miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa jengo hilo la utawala.

Pia, ametoa pongezi kwa uongozi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, kampasi ya Kijitonyama chini ya Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Joyce Nyoni, kwa usimamizi mzuri wa mradi huo kwa kutumia mapato ya ndani.

"Sisi kama kamati tumeridhishwa na maendeleo ya mradi huu na niwapongeze Mkuu wa Chuo, Dkt. Joyce Nyoni na Menejimenti ya Chuo cha Ustawi wa Jamii kwa kazi nzuri ya kusimamia mradi huo kwa fedha za ndani," amesema Mhe. Fatma Toufiq.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Dkt. Joyce Nyoni, amesema kuwa gharama za mradi huo ni shilingi Milioni 626.4 zikitokana na chanzo cha mapato ya ndani.

Aidha, Dkt. Nyoni amesema kuwa hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 35, ambapo ulianza Julai 22, 2024 na unatarajiwa kukamilika mnamo Julai 2025.

Akitoa neno la shukrani katika kikao hicho, Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, ameishukuru Kamati hiyo kwa kuendelea kutoa mwongozo mzuri kuhusu usimamizi wa miradi na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza.

"Tunapokea pongezi hizi kwa moyo wa shukrani na yale mliyotuelekeza tufanye marekebisho, sisi kama Wizara tumeyapokea na tutayafanyia kazi" Alisema Mhe. Mwanaid