Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

CHAKATENI TAARIFA ZA GEF KWA UADILIFU ILI ZIWEZE KUTUMIKA KWENYE TAARIFA YA TAIFA-Mhe.Kairuki.

Imewekwa: 20 Aug, 2025
CHAKATENI TAARIFA ZA GEF KWA UADILIFU ILI ZIWEZE KUTUMIKA KWENYE TAARIFA YA TAIFA-Mhe.Kairuki.

Na WMMJWM-Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Programu ya Kizazi chenye Usawa Mhe. Angela Kairuki amewataka waratibu wa Programu ya Kizazi chenye Usawa kuhakikisha wanakusanya taarifa zenye matukio chanya na changamoto zake na kuzichakata vizuri kwa ajili ya kurahisisha uaandaaji wa taarifa ya ujumla ya kitaifa.

Ameyasema hayo leo Agosti 6, 2025 jijini Dodoma wakati wa ahitimishaji Kongamano la Tathimini ya Utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa ngazi ya Mikoa na Hamashauri lililohudhuriwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii ambao ni waratibu wa Programu hiyo kutoka katika Halamashauri na Mikoa yote ya Tanzania pamoja na Wawakilishi kutoka Zanzibar.

“Niwapongeza washiriki wote kwa kuweza kuonesha ushirikano wakati wote wa Kongamano na kuweza kuwasilisha mafanikio chanya yaliyopatikana kwenye maeneo yao kupitia Programu ya kizazi chenye usawa na kuweza kuainisha fursa, maoni na changamoto zinazowakabili wakati wanatekeleza mradi huu ambazo zitasilishwa wizarani kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi” amesema Kairuki.

Kairuki ameeleza kuwa Programu hiyo inatarajia kufikia ukomo ifikapo Juni 2026 kwani huo ndiyo wakati muafaka ambapo jamii itatakiwa kufiki namna bora ya kuiendeleza ili kuimarisha usawa wa kijinsia na haki za kiuchumi kwa wanawake na wasichana kwenye kwenye halmashauri na mikoa pamoja na kushirikiana na vyombo vya habari kwa ajili ya kuwa na hadithi nzuri kuhusu Programu hiyo.

Aidha, Kairuki ametoa msisitizo kwa waratibu katika baadhi ya maeneo ambapo amegusia juu ya uzingatiaji wa malengo ya Programu ili kuhakikisha kunakua na uendelevu, kuhakikisha waratibu wanafanya thathimini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Programu pamoja kukamilisha taarifa zao, kudumisha ushirikiano na wadau hasa wa Asasi za kiraia, kijamii na makundi mengine ili kuweza kukamilisha malengo yaliyowekwa na kuanzisha utaratibu na utamaduni wa kujifunza baina ya Waratibu.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Zanzibar, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sitti Ali ameishuruku Wizara ya Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum kwa kufanikisha ushiriki.