Matukio

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

Mahali

MIKOA YOTE NCHINI

Tarehe

2023-06-16 - 2023-06-16

Muda

3:00 ASUBUHI - 7:00 MCHANA

Madhumuni

Katika kukumbuka siku hii, Umoja wa Nchi za Afrika mnamo mwaka 1991 uliweka Azimio la kuifanya siku ya tarehe 16 Juni ya kila mwaka kuwa siku maalum ya kuwaenzi mashujaa watoto waliokufa kwa ajili ya kudai haki yao ya kuendelezwa kielimu bila ubaguzi na hivyo kuitwa Siku ya Mtoto wa Afrika. Kuanzia hapo maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka katika nchi wanachama kwa kufanya tathmini kuhusu hali ya utoaji wa haki ya mtoto na huduma zinazohusu malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto.

Event Contents

Chimbuko la maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ni tukio la mauaji ya watoto takribani 2,000 yaliyofanywa na Askari wa Utawala wa Makaburu katika Kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini tarehe 16 Juni, 1976. Mauaji hayo yalitokea wakati Askari hao wanazuia maandamano ya watoto waliokuwa wanapinga mfumo wa elimu ya kibaguzi iliyokuwa inatolewa na Utawala wa Makaburu. Katika kukumbuka siku hii, Umoja wa Nchi za Afrika mnamo mwaka 1991 uliweka Azimio la kuifanya siku ya tarehe 16 Juni ya kila mwaka kuwa siku maalum ya kuwaenzi mashujaa watoto waliokufa kwa ajili ya kudai haki yao ya kuendelezwa kielimu bila ubaguzi na hivyo kuitwa Siku ya Mtoto wa Afrika. Kuanzia hapo maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka katika nchi wanachama kwa kufanya tathmini kuhusu hali ya utoaji wa haki ya mtoto na huduma zinazohusu malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto.

Kauli mbiu inayoongoza Maadhimisho ya mwaka huu, 2023 ni Zingatia Usalama wa Mtoto katika Ulimwengu wa Kidijitali”. Kauli mbiu hii inaelekeza watoto, wazazi na wanajamii kuchukua hatua za makusudi za kutetea haki za watoto zilizoainishwa katika Sera ya Mtoto (2008) ambazo ni Haki ya Kuishi, Kuendelezwa, Kulindwa, Kushiriki na Haki ya Kutobaguliwa kwa namna yoyote akiwa nyumbani, shuleni au kwenye jamii.

Aidha, siku hii inatukumbusha Wadau wote wa Watoto wajibu wetu wa kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili, hususani ukatili unaoibuka sasa hivi ambao ni ukatili wa kwenye mitandao unaotokana na matumizi yasiyo sahihi ya vifaa vya kielektroniki kwa kuingia kwenye mitandao na kujikuta wanafanyiwa ukatili wa aina mbalimbali ikiwemo vitisho na kurubuniwa au kushawishiwa kuonesha au kuonyeshwa maudhui ya ngono kwa njia ya picha au video. Aidha, hali hiyo hupelekea hata kufanyiwa au kufanyishwa vitendo vya kingono mitandaoni.

Washiriki

WANANCHI WOTE

Ada ya Tukio

BURE

Simu

+255 26 2963341/42/46

Barua pepe

ps@jamii.gotz