Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

WAZIRI GWAJIMA AZINDUA MWONGOZO WA USHIRIKI WA WADAU KATIKA MIKUTANO YA KIKANDA KIMAIFA.

Imewekwa: 11 May, 2026
WAZIRI GWAJIMA AZINDUA MWONGOZO WA USHIRIKI WA WADAU KATIKA MIKUTANO YA KIKANDA KIMAIFA.

Na, WMJJWM- Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima amezindua Mwongozo wa Kuratibu Ushiriki wa Wadau wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika Mikutano ya Kikanda na Kimataifa wa mwaka 2024 kwa lengo la kuhakikisha ushiriki wa Tanzania katika mikutano hiyo unakuwa na tija kwa taifa. Uzinduzi huo umefanyika tarehe 09 Mei, 2026 jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt. Gwajima amesema mwongozo huo umeandaliwa ili kuweka mfumo madhubuti wa usimamizi, uratibu, ufuatiliaji na tathmini ya ushiriki wa Serikali pamoja na wadau mbalimbali katika mikutano ya kikanda na kimataifa inayohusu maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum.

Amesema mwongozo huo utawezesha uratibu wa shughuli zote kabla, wakati na baada ya mikutano hiyo, hatua ambayo itaisaidia Wizara kufahamu aina ya mikutano inayoshirikishwa wadau wake pamoja na tija inayopatikana kwa maendeleo ya nchi.

Dkt. Gwajima ameongeza kuwa mafanikio ya ushiriki wa kimataifa yanategemea maandalizi madhubuti yanayojumuisha uandaaji wa ripoti za nchi, upatikanaji wa rasilimali fedha pamoja na ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ya kijamii yakiwemo wanawake, vijana, wanaume, wazee, wajane na viongozi wa serikali.

Naye Mhadhiri kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dkt. Sirieli Mchembe, akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa masuala ya usawa wa kijinsia amesema Tanzania inaendelea kutekeleza ajenda hiyo kupitia sera, mipango na mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kufikia usawa wa kijinsia ifikapo mwaka 2030 kwa kuzingatia Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Kikao hicho kimewakutanisha viongozi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, mashirika yasiyo ya kiserikali, wahandisi wanawake, majaji pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ya jinsia na wanawake nchini pamoja na Wizara za kisekta kwa lengo la kutathmini mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika mkutano wa CSW70 uliofanyika jijini New York mwezi Machi mwaka huu.

slot gacor