Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

WAZIRI DKT. GWAJIMA APONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO LUDEWA, AHIMIZA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI NA KUIMARISHA MAADILI

Imewekwa: 06 Jul, 2026
WAZIRI DKT. GWAJIMA APONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO LUDEWA, AHIMIZA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI NA KUIMARISHA MAADILI

Na Saidi Saidi, WMJJWM – Ludewa

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, ameipongeza Serikali ya Mkoa wa Njombe pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa kusimamia na kutekeleza kwa ufanisi miradi ya maendeleo inayoendelea kuboresha huduma kwa wananchi. Dkt. Gwajima amesema hayo Julai 4, 2026 wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mlagali katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Itundu, baada ya kutembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.

Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Gwajima ametolea mfano miradi ya afya na elimu aliyoitembelea na kuizindua, ikiwemo Jengo la Huduma za Mionzi (X-Ray), Zahanati ya Lihagule na madarasa mapya katika Shule ya Msingi Manda. Amesema miradi hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuendelea kuboresha huduma za kijamii na kuinua ustawi wa wananchi.

Aidha, Dkt. Gwajima Amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu na miradi ya maendeleo ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kusogeza huduma muhimu karibu yao.

Pamoja na hayo, Dkt. Gwajima amesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika maadili mema kwa watoto na vijana kupitia malezi na makuzi bora, akieleza kuwa ndiyo msingi wa kujenga rasilimali watu yenye tija kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mheshimiwa Olivanus Thomas, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo ambapo miradi hiyo imeendelea kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi.

Naye Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Mhe. Joseph Kamonga, ameishukuru Serikali kuendelea kuwekeza katika miradi ya maendeleo wilayani humo, huku akiiomba kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo ili kurahisisha  shughuli za kiuchumi na kijamii pamoja na kuchochea maendeleao.

slot gacor