Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

WAZIRI DKT. GWAJIMA AANZISHA KIPINDI MAALUMU CHA KUIELIMISHA JAMII KUHUSU HUDUMA ZA WIZARA

Imewekwa: 22 Jun, 2026
WAZIRI DKT. GWAJIMA AANZISHA KIPINDI MAALUMU CHA KUIELIMISHA JAMII KUHUSU HUDUMA ZA WIZARA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mheshimiwa Dkt. Dorothy Gwajima, ameanzisha kipindi maalumu kitakacholenga kuwaelimisha wananchi kuhusu majukumu, huduma, programu, sera na mafanikio ya Wizara hiyo.

Kupitia kipindi hicho, wananchi watapata fursa ya kuifahamu kwa undani Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, nafasi yake katika maendeleo ya Taifa, pamoja na namna huduma zake zinavyogusa maisha ya kila siku ya Watanzania.

Akiwa Kama mwendesha kipindi Dkt. Gwajima amesema kuwa Kipindi hicho kitawakutanisha wataalamu na viongozi wa Wizara watakaofafanua utekelezaji wa sera, miradi na huduma mbalimbali zinazohusu maendeleo ya jamii, ustawi wa jamii, jinsia, wanawake, watoto na makundi maalum. Aidha, kitatoa nafasi kwa wananchi kupata elimu, kuuliza maswali na kuelewa fursa mbalimbali zinazotolewa na Wizara.

Dkt. Gwajima amewataka wananchi kufuatilia kipindi hicho kupitia mitandao ya kijamii, ikiwemo YouTube Channel ya Dkt. Dorothy Gwajima pamoja na Jamii Yetu Tanzania, ili kupata elimu sahihi na kushiriki kikamilifu katika ajenda za maendeleo ya jamii.

slot gacor