WADAU WA MTAKUWWA WAELEKEZWA KUONGEZA JITIHADA ZA UTEKLEZAJI.
Na Abdala Sifi WMJJWM – Dodoma
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo Jamii wa Wizara ya Manendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Carlos Gwamagobe amewataka wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto, eneo la pili la mila na desturi, kuongeza jitihada na mbinu mbalimbali za kufikisha elimu kwa jamii.
Gwamagobe amesema hayo leo tarehe 5 Disemba, 2025 jijini Dodoma, wakati akifungua kikao cha robo ya kwanza cha wadau wa MTAKUWWA wanaotekeleza afua mbalimbali ili kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Amesema kikao hicho kimelenga kupokea taarifa za utekelezaji kutoka Wizara za kisekta na wadau wanaotekeleza afua mbalimbali za kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini.
Naye Mwalikilishi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Regina Kaaya ameleeza kwamba Wizara hiyo imeshaandaa mwongozo, mkakati na sera ya utamaduni inayohusu kupinga vitendo vya ukatili na tamaduni zenye madhara ambao utatekelezwa kupitia programu mbalimbali za michezo na sanaa.
Kwa upande wake Meneja Miradi kutoka Shirika la Mtoto Foundation Mbwana Mbwana, amesema wamefanikiwa kutoa elimu ya mabadiliko chanya kwa Watoto waliopitia ukatili wa kijinsia mkoani Tanga.
Naye Joseph Mbasaha kutoka Shirika la Help Age Tanzania amesema katika kutoa elimu ya kuachana na mila na desturi hasi wamekuwa wakiendesha mijadala ya wazi inayowahusisha wazee kwa ajili ya kujenga uelewa na kuibua changamoto ukatili dhidi ya Watoto na wanawake.
Baadhi ya njia zilizotajwa kutumika kuwasaidia waathirika wa vitendo vya ukatili ni kuwapa elimu za ujasiriamali ikiwemo kuwapatia mizinga ya ufugaji wa nyuki na kuku kwa lengo la kuwawezesha wanawake kukuza uchumi wa familia.
Njia nyingine ni uendeshaji wa mijadala ya wazi katika jamii kuhusu madhara ya mila desturi zenye madhara, elimu kwa jamii kupitia vipindi vya radio na Luninga pamoja na kuwashirikisha viongozi wa dini.
MWISHO