Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

SERIKALI YASISITIZA ULINZI NA HESHIMA KWA WAZEE.

Imewekwa: 16 Jun, 2026
SERIKALI YASISITIZA ULINZI NA HESHIMA KWA WAZEE.

SERIKALI YASISITIZA ULINZI NA HESHIMA KWA WAZEE.

Na, Oscar Tarimo -WMJJWM-KAGERA

Serikali imewataka wananchi, familia na viongozi wa jamii kuendelea kuwalinda wazee dhidi ya vitendo vya ukatili, unyanyasaji na ubaguzi, huku ikisisitiza kuwa wazee ni hazina ya Taifa na wadau muhimu katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Wito huo umetolewa na Kaimu Kamishina Msaidizi wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mussa Mkamate, alipomwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Chacha Maswi, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee yaliyofanyika 15 juni,2026 mkoani Kagera chini ya kaulimbiu isemayo “Zuia Ukatili Dhidi ya Wazee; Wajibika.”

Ameeleza kuwa pamoja na mchango huo mkubwa, wazee wengi bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ukatili, unyang’anyi wa mali na ardhi, kutengwa na familia, changamoto za afya pamoja na mashambulizi yanayotokana na imani potofu.

Mkamate amesisitiza kuwa wazee hawapaswi kutumiwa kuombaomba mitaani ilhali Serikali imeweka mifumo ya kuwahudumia wazee wasiojiweza. Alifafanua kuwa kwa sasa kuna makazi 13 ya wazee yanayoendeshwa na Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum pamoja na makazi 16 yanayomilikiwa na sekta binafsi ambayo yanatoa huduma za matunzo na hifadhi kwa wazee wanaohitaji msaada maalum.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Taifa, David Lameck Sendo, amesema wazee wana haki ya kulindwa, kuheshimiwa na kupata huduma bora za afya huku aksisitiza kuwa Baraza hilo litaendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kutetea haki na maslahi ya wazee nchini ili kuhakikisha wanaishi maisha yenye utu, usalama na heshima inayostahili.

Naye mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Yohana Sima aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhani Kido, amesema jamii ina wajibu wa kuhakikisha wazee wanapata mazingira salama na yenye heshima.

slot gacor