Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

SERIKALI YAHAKIKISHA MAZINGIRA BORA KATIKA MAKAZI YA WATOTO NCHINI.

Imewekwa: 25 May, 2026
SERIKALI YAHAKIKISHA MAZINGIRA BORA KATIKA MAKAZI YA WATOTO NCHINI.

Na Jackline Minja, Dodoma

Serikali imeendelea kuweka utaratibu madhubuti wa kuhakikisha watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto wanakuwa katika mazingira bora, salama na yenye kuzingatia ustawi wao kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Lucy Simirya Kombani, aliyetaka kujua Serikali imejipangaje kuhakikisha watoto wanaoishi kwenye vituo vya kulelea watoto wanaishi katika mazingira bora na salama.

Mahundi amesema Makao ya Watoto nchini yanaanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Sura ya 13, Kanuni za Makao ya Watoto za mwaka 2012 pamoja na Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji, Uendeshaji na Usimamizi wa Makao ya Watoto wa mwaka 2024.

"Utaratibu wa usajili wa makao hayo huanzia katika ngazi ya Kata na Halmashauri kabla ya kuwasilishwa Wizara husika kupitia Kamishna wa Ustawi wa Jamii kwa ajili ya kupata leseni ya usajili baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa aidha Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka ngazi ya Wizara, Mkoa na Halmashauri wanaendelea kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa mara kwa mara katika makao hayo ili kuhakikisha watoto wanapatiwa huduma bora za malezi, ulinzi na usalama wakati wote". Aliseme Mhe Mahundi

Serikali imeeleza kuwa hatua hizo ni sehemu ya dhamira ya kuhakikisha watoto wote wanaolelewa katika vituo mbalimbali wanapata haki zao za msingi na kukua katika mazingira yenye upendo, malezi bora na usalama.

slot gacor