MPANJU APONGEZA SHIRIKA LA SALT
Na WMJJWM Dar Es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju amelipongeza Shirika la Stategic Alitenative Learning Techniques (SALT) amabo limejikita katika kuhudumia watoto wenye Usonji.
Mpanju ametoa pongezi hizo Aprili 12, 2026 baada ya kukabidhi zawadi na mahitaji mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya watoto hao.
Wakili Mpanju amesema huduma wanayotoa inagusa maisha ya watoto wengi, hivyo Serikali inakupongeza kwa juhudi hizo na itaendelea kutoa ushirikiano ili kuweza kuhudumia watoto wengi zaidi.
Naye Mkurugenzi wa Shirika hilo Rebecca Labi ameishukuru Serikali kupitia Wakili Mpanju kwa kuwatembelea na kuwapatia mahitaji mbalimbali kwa ajili ya watoto hao.
Ziara hiyo ilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani iliyofanyika Aprili 12, 2026 katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli Mbezi.