Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MHE. MAHUNDI ATOA WITO WA KUENDELEZA MAADILI KUPITIA MUZIKI WA INJILI.

Imewekwa: 08 Jun, 2026
MHE. MAHUNDI ATOA WITO WA KUENDELEZA MAADILI KUPITIA MUZIKI WA INJILI.

Na Jackline Minja, Dar Es Salaam

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Maryprisca Mahundi, ametoa wito kwa jamii kuendeleza maadili kupitia muziki wa injili katika nyumba mbalimbali za ibada.


Mhe. Mahundi ameyasema hayo leo Juni 6, 2026 akishiriki katika hafla ya uzinduzi wa albamu ya Santuli “Unataka kuwa ?” ya Kwaya ya Mabwepande Central SDA Choir iliyofanyika katika Kanisa la Waadventista Wasabato Mabwepande, mkoani Dar Es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Mahundi amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za dini katika kujenga jamii yenye maadili, mshikamano na matumaini kupitia huduma mbalimbali ikiwemo muziki wa injili.

Amesema muziki ni nyenzo muhimu ya kuelimisha jamii, kuimarisha maadili mema na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo.

"Niwapongeze Kwaya ya Mabwepande Central SDA Choir kwa juhudi zanu za kuhubiri Injili kupitia uimbaji na kwa kuendelea kushiriki katika shughuli za kijamii zikiwemo kuwasaidia wenye uhitaji, yatima na makundi mbalimbali yanayohitaji msaada katika jamii." amesema Mhe. Mahundi

Aidha, amepongeza hatua ya kwaya hiyo kufanikisha uzinduzi wa albamu hiyo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza huduma ya kiroho na kijamii kwa wananchi. 

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kuhamasisha maadili mema, amani na mshikamano wa kitaifa, huku akiwataka wanakwaya na waumini kuendelea kutumia vipaji vyao kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, uongozi wa Kwaya ya Mabwepande Central SDA Choir umeeleza kuwa albamu ya “Unataka kuwa ?” inalenga kueneza ujumbe wa Injili, kuimarisha imani za waumini na kuhamasisha jamii kuzingatia maadili mema na kuomba wadau mbalimbali kuendelea kuiunga mkono kwaya hiyo katika jitihada zake za kuimarisha huduma ya uimbaji na shughuli za kijamii. 

slot gacor