Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

DKT. GWAJIMA AZINDUA TAWASIFU YA “NIMEWEZA”, AHIMIZA UTAMADUNI WA KUANDIKA.

Imewekwa: 08 Jun, 2026
DKT. GWAJIMA AZINDUA TAWASIFU YA “NIMEWEZA”, AHIMIZA UTAMADUNI WA KUANDIKA.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amehimiza Watanzania kuendeleza utamaduni wa kuandika na kuhifadhi historia za maisha yao kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Tawasifu ya NIMEWEZA iliyoandikwa na Mhe. Mwalimu Queen Mwanshinga Mlozi, tarehe 6 Juni, 2026 Jijini Dodoma.

Amesema kitabu hicho ni zaidi ya simulizi ya maisha ya mwandishi wake kwani kinafunua maadili, misingi ya uongozi, ustahimilivu na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.

Dkt. Gwajima amempongeza Mhe. Queen Mwanshinga Mlozi kwa hatua ya kuandika tawasifu hiyo, akieleza kuwa ametoa mchango mkubwa katika kuhifadhi historia na kuhamasisha wanawake wengine kuthubutu kuandika safari zao za maisha na mafanikio huku akisisitiza kuwa uandishi wa tawasifu ni njia muhimu ya kurithisha maarifa, ujuzi na tajiriba kwa jamii.

“Ninahimiza watu kuandika kila mtu ana hadithi yake ya maisha ambayo inaweza kuwasaidia wengine kujifunza, kupata hamasa na kuchangia maendeleo ya jamii.” amesema Dkt. Gwajima.

Kwa upande wa maendeleo ya jamii, Waziri Dkt. Gwajima amesema tawasifu ya NIMEWEZA imebeba mafunzo yanayoweza kusaidia kuimarisha taasisi ya familia, elimu, uongozi na mifumo ya utawala katika ngazi mbalimbali kwani changamoto nyingi za kijamii zinazoikabili jamii zinaanzia katika taasisi ya familia, hivyo maudhui ya kitabu hicho yana mchango mkubwa katika kujenga familia imara na jamii yenye ustawi.

Kwa upande wake, Mwandishi wa Tawasifu ya NIMEWEZA, Mhe. Mwalimu Queen Mwanshinga Mlozi, amesema uamuzi wa kuandika kitabu hicho umetokana na dhamira ya kushirikisha jamii uzoefu, mafunzo na changamoto mbalimbali alizokutana nazo katika maisha na safari yake ya uongozi huku akieleza wasifu huo unaelezea hatua mbalimbali alizopitia tangu utotoni, katika elimu, maisha ya familia na nyadhifa mbalimbali za uongozi alizowahi kuzishika.

 

slot gacor