Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

WAANDISHI WA HABARI REDIO JAMII WAPIGWA MSASA KAMPENI YA INSPIRE TO LEAD

Imewekwa: 17 Feb, 2026
WAANDISHI WA HABARI REDIO JAMII WAPIGWA MSASA KAMPENI YA INSPIRE TO LEAD

WAANDISHI WA HABARI REDIO JAMII WAPIGWA MSASA KAMPENI YA INSPIRE TO LEAD

 

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka katika Redio za Kijamii kuhusiana na utayarishaji wa jumbe za kubadilisha mtazamo wa jamii kwenye suala zima la usawa wa kijinsia, kupambana na ukatili, kutumia fursa uwezeshwaji kiuchumi  pamoja na kuhamashisha wanawake kushiriki katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi na maamuzi katika jamii.

 

Mafunzo haya ya siku mbili yanafanyika tarehe 17 -18, Februari, 2026 jijini Mwanza na yamehudhuriwa pia na Wataalam wa Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Maafisa Habari na Wataalam wa kada nyingine zinazohusika katika kutoa huduma kwa jamii.