Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM YA SHILINGI BILIONI 108.

Imewekwa: 02 Jun, 2026
BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM YA SHILINGI BILIONI 108.

Na Oscar Tarimo-WMJJWM-Dodoma,

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa mwaka wa fedha 2026/27 yenye jumla ya Shilingi bilioni 108.024 kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa jamii nchini.

Bajeti hiyo imepitishwa baada ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, kuwasilisha hotuba ya mapitio ya utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27.

Akiwasilisha hotuba hiyo bungeni jijini Dodoma, Dkt. Gwajima amesema Wizara itaendelea kutekeleza vipaumbele vya kimkakati vinavyolenga kujenga mtaji watu wa Taifa, kuimarisha malezi na makuzi ya watoto, kukuza usawa wa kijinsia, kuwawezesha wanawake na makundi maalum kiuchumi pamoja na kuimarisha ustawi wa jamii.

Amesema katika mwaka wa fedha 2025/26, Wizara imeendelea kupata mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo usajili wa wafanyabiashara ndogondogo, utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu, uimarishaji wa huduma za ustawi wa jamii, malezi ya watoto pamoja na uratibu wa afua za kutokomeza ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.

Aidha, Wizara imeendelea kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo kupitia kampeni mbalimbali za maendeleo ya jamii, huku ikiimarisha huduma kwa wazee, watoto, wanawake na makundi mengine maalum kwa lengo la kujenga jamii yenye ustawi na maendeleo jumuishi.

Kwa mujibu wa makadirio yaliyopitishwa, kiasi cha Shilingi bilioni 50.138 kimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 57.886 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo itakayochangia kuboresha huduma za kijamii na ustawi wa wananchi nchini.

Kupitishwa kwa bajeti hiyo kunatarajiwa kuiwezesha Wizara kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi na kuchochea maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kwa wananchi wote, sambamba na kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 20

slot gacor