
MALEZI
Wizara kwa kushirikiana na Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Tanzania (TECDEN) na Mtandao wa Malezi Afrika (AfECN), inatekeleza Kampeni ya Kitaifa ya Malezi ya Watoto Wadogo nchini kwa mwaka 2024/25 hadi 2025/26. Kampeni hii ni sehemu ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) na inalenga kuhamasisha jamii nzima kuhusu umuhimu wa huduma bora za malezi kwa watoto walio na umri wa miaka 0 hadi 5. Lengo la kampeni hii ni kukuza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa malezi bora kwa watoto wadogo kwa kuwashirikisha familia, watunga sera, viongozi wa serikali na jamii, sekta binafsi, na wadau wa maendeleo ili kuongeza uwekezaji katika huduma za malezi jumuishi, nafuu, na bora kwa watoto wote nchini.