
ULINZI NA USALAMA WA MTOTO MTANDAONI
Wizara inaratibu kampeni ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto mtandaoni ambayo ilizinduliwa februari,2024. Kampeni hii ilitokana na utafiti ya hali ya ukatili wa Watoto mtandaoni wa mwaka 2022 (Distrupting Harm Report). Utafiti ulionyesha kuwa 67% ya Watoto wa miaka 12-17 wanatumia mitandao. kati yao 4% walishawahi kufanyiwa ukatili wa aina mbalimbali mtandaoni ikiwemo kurubuniwa,kutishwa na kulazimishwa ngono, 5% walishawahi kulazimishwa kutuma picha zao za utupu. Kampeni hii inategemea kufika Mikoa yote Tanzania Bara. Lengo la kampeni ni kuhamasisha Wazazi/ Walezi, Walimu, Watoto na Jamii kwa ujumla kuhusu matumizi yasiyofaa ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa Watoto