Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

AMASHA ARI
AMASHA ARI

Kampeni ya amsha ari ni mahsusi kwa ajili ya kubadilisha na kugeuza fikra, mitazamo na mawazo ya wananchi ili wawe chachu na kitovu cha maendeleo ndani ya jamii wanayoishi. Wananchi wakishirikishwa  ipasavyo watakuwa mstari wa mbele kusimamia maendeleo yanayotekelezwa ndani ya jamii yao ikiwa ni sambamba na kuihifadhi miradi ya maendeleo ili iweze kudumu kwa vizazi vingi zaidi. Lengo la kampeni hii ni kufanya mageuzi ya kifikra na mtazamo wa jamii kuwa na moyo wa kujitegemea, uzalendo na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo endelevu na jumuishi.