
KUTOKOMEZA UKEKETAJI NCHINI
Wizara inaratibu na kusimamia utekelezaji wa kampeni ya Kitaifa ya kupinga ukeketaji kwa mwaka 2020/2030. Kampeni hii ni utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA). Lengo ni kufikisha elimu kwa jamii kuachana na mila zenye madhara kwa watoto wa kike na wanawake pamoja na kuwapa msaada na huduma Manusura na Wahanga wa Ukeketaji.